Zaidi ya Malori 40 yaliyokuwa yakipeleka mizigo katika nchi za Burundi na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo,yamejikuta yakikwama kwa muda wa masaa zaidi ya 18 katika kijiji cha Murugarama baada ya Lori moja wapo kuanguka na kufunga barabara.
Lori hilo lenye namba za usajiri T 700 BFS lilianguka majira ya saa nane mchana siku ya jumapili April 15 katika kijiji cha Murugarama eneo la Njiapanda ya Rulenge,ambapo lilikuwa likipeleka mahindi nchini Burundi,na baada ya kuanguka lilifunga barabara hiyo hali iliyopelekea magari mengi hasa malori kukosa njia ya kupita kwa masaa kadhaa.
Watu walioshuhudia ajali hiyo wamesema kuwa chanzo chake ni mwendo wa kasi wa gari hilo,pamoja na mvua iliyokuwa ikinyesha kwa muda mrefu katika eneo hilo na kusababisha utelezi.
Hata hivyo watu waliokuwa katika gari hilo walisalimika ambao ni dereva na utingo.
Gari hilo awali likuwa likimilikiwa na Bw.Tenth Maruhe mkazi wa mjini Ngara kabla ya kuliuza kwa Mbarakk wa Biharamulo.
 |
jitihadazikiendelea za kuliondoa barabarani |
Baada ya madereva hao kuona hakuna jitihada zozote zinazofanywa na mamlaka husika kuondoa gari hilo barabarani,walishirikiana wao wenyewe na kulitoa ambapo shughuli za usafirishaji katika barabara hiyo zimelejea katika hali ya kawaida.
 |
hivi ndivyo lilivyokaa baada ya kuanguka |
 |
wananchi wakishirikiana kuinua tela la lori hilo |
Ajali hiyo ni ya pili kutokea katika eneo hilo kwa kipindi cha miezi miwili,ambapo mwezi wa pili watu wawili walipoteza maisha baada ya kugongwa na roli katika eneo hilo hilo.