Maadhimisho ya wiki ya maji wilayani Ngara yalimalizika wiki iliyopita kwa Mkuu wa wilaya ya Ngara Kanali msitaafu Salum Nyakonji kuwataka wananchi wote wanaofanya shughuli za kibinadamu kando mwa vyanzo vya maji kusitisha shughuli hizo mara moja vinginevyo nguvu ya sheria itatumika kwa wale watakaokaidi agizo hilo.
Akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Ngara Salum Nyakonji,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Bw.John Nshimimana alisema kuwa serikali wilayani Ngara iko na wananchi bega kwa bega ili kuhakikisha wananchi wote wa wilaya hiyo wanapayta maji safi na salama.
mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Mh.John Nshimimana akizindua tenki la maji kwa niaba ya mkuu wa wilaya katika kata ya Ntobeye,kulia ni diwani wa kata hiyo Mh.John Ruzige. |
wanafunzi wa shule ya msingi Ntobeye wakitumbuiza katika kilele cha wiki ya maji |
Maadhimisho hayo yalizinduliwa katika kijiji cha Ntelungwe kata ya Nyamiaga,na baada ya hapo zilifuatia shughuli mbali mbali za kimaendeleo katika sekta ya maji wilayani kote,ikiwa ni pamoja na kukagua miradi ya maji na kuzindua miradi hiyo.
No comments:
Post a Comment