"VIJANA NGARA ACHENI USHABIKI WA VYAMA VYA SIASA,TUJIPANGE KUELEKEA MCHAKATO WA KATIBA MPYA."
Vijana wilayani Ngara mkoani
Kagera,wametakiwa kuacha ushabiki wa vyama vya siasa na badala yake wajitokeze
kwa wingi kutoa maoni yao
kuhusu uundwaji wa katiba mpya,pindi muda utakapofika wa kufanya hivyo.
Rai hiyo imetolewa na katibu
wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wilayani Ngara Bw.Joseph
Milenzo,alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hizi.
Amesema kwa sasa vijana wengi
wameingia katika ushabiki wa kisiasa,hali ambayo inaweza kusababisha kutolewa
kwa maoni ya kishabiki mpaka kupelekea katiba mpya isiwe na maslahi kwa vijana
Bw. Milenzo amesema kuwa
katiba ndio muongozo wa taifa,hivyo vijana wajitokeze kutoa maoni sahihi ili katiba itakayoundwa
iweze kukidhi mahitaji yao.
Katibu huyo wa UVCCM ameonyeshwa kukerwa sana na tabia za
baadhi ya vijana wengi kuwa mashabiki wa vyama vya siasa hasa upinzani,huku
wengi wao wakiwa hawana sababu za msingi zaidi ya ushabiki tu.
No comments:
Post a Comment