Wananchi wilayani hapa,wametakiwa kutumia maji safi katika shughuki mbali mbali na sio kupikia tu.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu tawala wa wilaya ya Ngara Bw.Erasmus Rugarabamu,alipokuwa akikabidhi mradi wa maji safi katika kijiji cha Mukalinzi kata ya Muganza wilayani Ngara.
Ikiwa ni katika maadhimisho ya wiki ya maji,Bw.Rugarabamu amesema kuwa wananchi wengi wa wilaya hiyo,wamekuwa wakitumia maji safi kwenye kupikia tu,wakati wao na watoto wao wamekuwa hawajali suala la usafi kwa kufulia nguo maji mengi yanayopatikana wilayani humo.
![]() |
katibu tawala wa wilaya ya Ngara Bw.Erasmus Rugarabamu,akizindua rasmi mradi wa maji safi katika kijiji cha mukalinzi kata ya Muganza. |
Kwa upande wao wananchi wa kijiji hicho wameishukuru serikali kuweza kuwafikishia mradi wa maji safi,kwani awali walikuwa wakittumia kisima ambacho kilikuwa katika hali mabaya sana kiafya.Mradi huo umejengwa na shirika la TWESA kwa ufadhili wa CONCERN WORLD WIDE,ambapo utakuwa unahudumia zaidi ya kaya 80 za kijiji hicho.
![]() |
hiki ndicho kisima ambacho awali kilikuwa kikitumiwa nawananchi hao |
No comments:
Post a Comment