ASHTAKIWA KWA KOSA LA MAUAJI
Mkazi wa
kijiji cha chivu wilayani Ngara mkoani kagera amefikishwa katika mahakama ya
wilaya hiyo kwa kosa la mauaji.
Mshitakiwa Laurian Philemon mwenye umri wa miaka 27 mkazi wa kijiji cha
chivu wilayani Ngara anatuhumiwa kutenda kosa hilo march
7 mwaka huu majira ya saa nne usiku
kijijini hapo
Mbele ya
mlinzi wa amani bw Andrew kabuki, mwendesha mashitaka wa Polisi Bw Tumaini
Mumbi amesema mshitakiwa anadaiwa kumuua Bi, Marysiana Leonard aliyekuwa mkazi
wa kijiji cha chivu
Mshitakiwa
hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa alikuwa mbele ya mlinzi wa amani ambapo
amepelekwa rumande na kesi hiyo itatajwa tena
march 29 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment