WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA
Watu wawili
wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja baada ya kupatikana
na hatia katika kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha
Hakimu wa
mahakama ya wilaya ya Ngara Bw Idrisa Katela ametoa hukumu hiyo dhidi ya Athumani
Edd mkazi wa Nakatunga na Ladsilaus Onesimo mkazi wa kabanga wilayani Ngara
Awali mwendesha
mashitaka wa Polisi Bw Tumaini Mumbi alisema washitakiwa walimchoma kisu
kifuani Bw Lusinzi Sebabili na kumpora pikipiki yake na kuificha kwa Cosmas
Reveliani mkazi wa kabanga
Hata hivyo
Mshitakiwa Cosmas Relevian ameachwa huru baada ya kukosekana kwa ushahidi dhidi
yake
No comments:
Post a Comment