ALEX GASHAZA ATANGAZA KUGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA NGARA.
Kada wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Ngara Bw Alex Gashaza ametangaza rasmi kugombea uenyekiti wa wilaya wa chama hicho.
Bw.Gashaza ambaye amewahi kushiriki katika chaguzi kadhaa za ubunge wa jimbo la Ngara kupitia tiketi ya CCM mara mbili na mara moja kupitia tiketi ya NCCR Mageuzi,ameweka uamuzi huo hadharani katika kikao cha madiwani wa chama cha Mapinduzi kilichofanyika katika ofisi za CCM mjini Ngara.
Uchaguzi wa nafasi mbali mbali ndani ya CCM unafanyika mwaka huu ambapo kwa hivi sasa nafasi hiyo ya mwenyekiti inashikiliwa na Bi.Helena Adrian ambaye anamiliki shule ya RHEC iliyoko Rulenge
No comments:
Post a Comment