Wednesday, April 18, 2012

JAMBAZI AUWAWA NA POLISI


Diwani wa kata ya Kabanga MH SAID SOUD
Jeshi la polisi wilayani Ngara limemuua mtu anayedhaniwa kuwa jambazi aliyekuwa na bomu la kutupwa kwa mkono

Diwani wa kata ya Kabanga Bw. Said Ramadhani Soud amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Nzaza baada ya kundi la majambazi  kutoka Burundi kuvamia katika kijiji cha Murukukumbo

Amesema jeshi la polisi kituo cha kabanga lilipata taarifa hizo ambapo waliwafuatilia na kumuua jambazi huyo baada ya tukio la kurushiana risasi na majambazi hao.

Amesema jambazi aliyeuwawa amefahamika kwa jina la Erick Ndabiholele mwenyeji wa wilaya ya Murama nchini Burundi

Amesema Polisi wamepata vitu vyenye thamani ya shilingi laki mbili ikiwa ni pamoja na simu tatu za mkononi zilizokuwa zimeibwa na watu hao

Kata ya Kabanga imekuwa ikikumbwa sana na vitendo vya ujambazi wa kutumia silaha siku za hivi karibuni,ambapo zaidi ya watu wawili wameuwawa na majambazi hao tangu mwanzoni mwa mwaka huu,na inasemekana majambazi hao wanatoka nchi jirani ya Burundi

No comments:

Post a Comment