Halmashauri ya wilaya ya Ngara imenunua piki piki za magurudumu matatu zitakazokuwa zikifanya huduma ya kuwasafirisha wanawake wajawazito kutoka vijijini kuwapeleka sehemu za barabarani ambapo watakuwa wakichukuliwa na magari kuelekea katika hospitali kubwa za wilaya kwa ajili ya kupatiwa huduma za kiafya.
Akiongea na NGARALIVE Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Ngara Dk.David Mapunda,amesema piki piki hizo tatu zitapangiwa vituo ambavyo zitakuwa zikikaa,japo kwa sasa vityuo hivyo bado havijabainishwa.
mojawapo ya piki piki hizo ikiwa imeegeshwa katika hospitali ya Nyamiaga ikisubiri kupangiwa kituo.Hii itafika kweli Ntobeye kupitia njia ya Murgwanza? |
Dk.Mapunda ameongeza kuwa piki piki hizo ni kwa ajili ya wajawazito pekee tofauti na dharula nyingine zinazoweza kujitokeza
No comments:
Post a Comment