Mteremko wa K 9 umezidi kuwa tishio hasa kwa madereva wa maroli baada ya hivi karibuni lori moja kufail break kisha kuacha njia na kuua watu wawili papo hapo.
Dereva wa Lori hilo lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Burundi,ni mmoja kati ya waliopoteza maisha.
Mwingine ni mwendesha piki piki ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kasharazi,yeye alikuwa barabarani ambapo gari hilo lilimpitia katika harakati za kuacha njia.
hiyo ni sehemu ya CABIN ya lori hilo |
kwa mbali hiyo inayoonekana ndiyo piki piki iliyogongwa ikiwa chini ya gari hilo |
hivyo ndivy lilivyokuwa |
hilo ndilo container la gari hilo,lenyewe lilichomoka na kuporomoka zaidi ya mita mia moja hamsini,na ndani ya container hilo kulikuwa na gari jipya aina ya FUSO |
Utingo wa Lori hilo alishuka kuweka kigingi baada ya kuona kuwa limefail break,hivyo yeye hakuweza kupata jeraha lolote.
No comments:
Post a Comment