Thursday, March 29, 2012

WIKI YA MAJI

Askofu wa kanisa la Anglikana dayosisi ya Kagera Dk.Aron Kijanjali akipanda mti rafiki wa maji katika chanzo kipya cha maji safi cha Mubwilinde,baada ya kuzindua mradi huo.
Katibu wa TUMAINI FUND ambao ndio wamefanikisha ujenzi wa mradi wa maji safi katika kijiji cha Mubwilinde Bw.David Kibenza,akipanda mti rafiki wa maji kando ya chanzo hicho mara baada ya Askofu Kijanjali kuufungua mradi huo.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mubwilinde wakitoa burudani kwa watu waliohudhuria uzinduzi wa mradi wa maji safi katika kijiji cha Mubwilinde

WIKI YA MAJI

Askofu wa kanisa la Anglikana dayosisi ya Kagera Dk.Aron Kijanjali akiwaongoza mamia ya wakazi wa kijiji cha Mubwilinde katika sala kabla ya kuzindua mradi wa maji safi kwa wakazi wa kijiji hicho.Mwanzo kushoto ni Mratibu wa mradi huo ambaye ni katibu wa mfuko wa Tumaini Bw.David Kibenza
Askofu wa kanisa la Anglikana dayosisi ya Kagera Dk.Aron Kijanjali akifungua mradi wa maji katika kijiji cha Mubwilinde kata ya Bukiriro wilayani Ngara.Mradi huo umejengwa kwa ufadhili wa kanisa hilo kupitia Mfuko wa Tumaini.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mubwilinde ambao pia watanufaika na mradi huo wakifuatilia kwa makini wakati Askofu Kijanjali alipokuwa akifungua mradi huo.
Wananchi wa kijiji cha Mubwilinde wakifurahia kwa ngoma baada ya kujengewa mradi wa maji safi na salama

Monday, March 26, 2012

WIKI YA MAJI EXCLUSIVE

Maadhimisho ya wiki ya maji wilayani Ngara yalimalizika wiki iliyopita kwa Mkuu wa wilaya ya Ngara Kanali msitaafu Salum Nyakonji kuwataka wananchi wote wanaofanya shughuli za kibinadamu kando mwa vyanzo vya maji kusitisha shughuli hizo mara moja vinginevyo nguvu ya sheria itatumika kwa wale watakaokaidi agizo hilo.


Akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Ngara Salum Nyakonji,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Bw.John Nshimimana alisema kuwa serikali wilayani Ngara iko na wananchi bega kwa bega ili kuhakikisha wananchi wote wa wilaya hiyo wanapayta maji safi na salama.

mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Mh.John Nshimimana  akizindua tenki la maji kwa niaba ya mkuu wa wilaya katika kata ya Ntobeye,kulia ni diwani wa kata hiyo Mh.John Ruzige.
wanafunzi wa shule ya msingi Ntobeye wakitumbuiza katika kilele cha wiki ya maji
Hao ni wanasanaa kutoka katika kikundi cha Sanaa Kirushya,akina Baba Mpito na mama Mpito ambao wavuta hisia za umati wa watu waliokusanyika katika viwanja vya shule ya msingi Ntobeye katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji.

Maadhimisho hayo yalizinduliwa katika kijiji cha Ntelungwe kata ya Nyamiaga,na baada ya hapo zilifuatia shughuli mbali mbali za kimaendeleo katika sekta ya maji wilayani kote,ikiwa ni pamoja na kukagua miradi ya maji na kuzindua miradi hiyo.

Tuesday, March 20, 2012

   HATA SISI TUMO
Swala la utandawazi limeonekana kuingia sehemu kubwa ya dunia hata vijijini ambako zamani walikuwa wakipata habari baada ya mwezi mmoja.

Kwa sasa hali ni tofauti kwani wananchi wengi wamepata uwezo wa kumiliki vifaa vya habari kama vile Radio hata madish kama Camera yetu ilivyokuta huko katika kijiji cha Chivu.

Hii ni nyumba iliyokutwa tulioiona huko Chivu na wanamiliki satellite dish kwa ajili ya kupata kianchoendelea duniani.


hii ni nyumba iliyoko huko katika kijiji cha chivu
MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI WILAYANI NGARA.

Wananchi wilayani hapa,wametakiwa kutumia maji safi katika shughuki mbali mbali na sio kupikia tu.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu tawala wa wilaya ya Ngara Bw.Erasmus Rugarabamu,alipokuwa akikabidhi mradi wa maji safi katika kijiji cha Mukalinzi kata ya Muganza wilayani Ngara.

Ikiwa ni katika maadhimisho ya wiki ya maji,Bw.Rugarabamu amesema kuwa wananchi wengi wa wilaya hiyo,wamekuwa wakitumia maji safi kwenye kupikia tu,wakati wao na watoto wao wamekuwa hawajali suala la usafi kwa kufulia nguo maji mengi yanayopatikana wilayani humo.

katibu tawala wa wilaya ya Ngara Bw.Erasmus Rugarabamu,akizindua rasmi
mradi wa maji safi katika kijiji cha mukalinzi kata ya Muganza.
Kwa upande wao wananchi wa kijiji hicho wameishukuru serikali kuweza kuwafikishia mradi wa maji safi,kwani awali walikuwa wakittumia kisima ambacho kilikuwa katika hali mabaya sana kiafya.Mradi huo umejengwa na shirika la TWESA kwa ufadhili wa CONCERN WORLD WIDE,ambapo utakuwa unahudumia zaidi ya kaya 80 za kijiji hicho.

Friday, March 16, 2012


 ASHTAKIWA KWA KOSA LA MAUAJI
Mkazi wa kijiji cha chivu wilayani Ngara mkoani kagera amefikishwa katika mahakama ya wilaya hiyo kwa kosa la mauaji.

Mshitakiwa  Laurian Philemon  mwenye umri wa miaka 27 mkazi  wa kijiji cha  chivu  wilayani Ngara  anatuhumiwa kutenda kosa hilo  march 7 mwaka huu majira ya  saa nne usiku kijijini hapo

Mbele ya mlinzi wa amani bw Andrew kabuki, mwendesha mashitaka wa Polisi Bw Tumaini Mumbi amesema mshitakiwa anadaiwa kumuua Bi, Marysiana Leonard aliyekuwa mkazi wa kijiji cha chivu

Mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa alikuwa mbele ya mlinzi wa amani ambapo amepelekwa  rumande  na kesi hiyo itatajwa  tena  march 29 mwaka huu.


Thursday, March 15, 2012

                  
Mtangazaji wa Redio Kwizera SEIF OMAR UPUPU akizishangaa zana zilizokuwa zikitumika  zamani alipotembelea moja ya banda katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika viwanja vya posta wilayani Ngara.

Wednesday, March 14, 2012

WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA


Watu wawili wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia katika kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha

Hakimu wa mahakama ya wilaya ya Ngara Bw Idrisa Katela ametoa hukumu hiyo dhidi ya Athumani Edd mkazi wa Nakatunga na Ladsilaus Onesimo mkazi wa kabanga wilayani Ngara

Awali mwendesha mashitaka wa Polisi Bw Tumaini Mumbi alisema washitakiwa walimchoma kisu kifuani Bw Lusinzi Sebabili na kumpora pikipiki yake na kuificha kwa Cosmas Reveliani mkazi wa  kabanga

Hata hivyo Mshitakiwa Cosmas Relevian ameachwa huru baada ya kukosekana kwa ushahidi dhidi yake 
"VIJANA NGARA ACHENI USHABIKI WA VYAMA VYA SIASA,TUJIPANGE            KUELEKEA MCHAKATO WA KATIBA MPYA."


Vijana wilayani Ngara mkoani Kagera,wametakiwa kuacha ushabiki wa vyama vya siasa na badala yake wajitokeze kwa wingi kutoa maoni yao kuhusu uundwaji wa katiba mpya,pindi muda utakapofika wa kufanya hivyo.

Rai hiyo imetolewa na katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wilayani Ngara Bw.Joseph Milenzo,alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hizi.

Amesema kwa sasa vijana wengi wameingia katika ushabiki wa kisiasa,hali ambayo inaweza kusababisha kutolewa kwa maoni ya kishabiki mpaka kupelekea katiba mpya isiwe na maslahi kwa vijana

Bw. Milenzo amesema kuwa katiba ndio muongozo wa taifa,hivyo vijana wajitokeze  kutoa maoni sahihi ili katiba itakayoundwa iweze kukidhi mahitaji yao.                                                                                   

Katibu huyo wa UVCCM ameonyeshwa kukerwa sana na tabia za baadhi ya vijana wengi kuwa mashabiki wa vyama vya siasa hasa upinzani,huku wengi wao wakiwa hawana sababu za msingi zaidi ya ushabiki tu.