Monday, April 16, 2012

WANAFUNZI SITA TU DARASA ZIMA

jengo la utawala la shule ya sekondari MCHUNGAJI MWEMA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida shule ya Sekondari inayomilikiwa na kanisa la Anglikana dayosisi ya Kagera,MCHUNGAJI MWEMA,Imeonekana kupoteza kabisa mvuto kwa jamii baada ya shule hiyo kuwa na wanafunzi sita peke yao walioingia kidato cha kwanza mwaka huu shuleni hapo.

wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari MCHUNGAJI MWEMA wakiendelea na mjadala wa kimasomo darasani
Habari zilizoifikia NGARALIVE zinasema kuwa uhaba huo wa wanafunzi wanaojiunga na shule hiyo umepelekewa na matokeo mabovu ya kidato cha nne kwa mwaka jana hali ambayo imewakatisha tamaa wazazi.


Nao wanafunzi wa shule hiyo wamesema kuwa hali hiyo inachangiwa na kutokuwepo na maelewano mazuri kati ya waalimu wa shule hiyo na uongozi wa Dayosisi ya Kagera ambao ndio wamiliki wa shule hiyo.

1 comment:

  1. Nimefundisha hapo kwa zaidi ya miaka 3 lakini, jinsi Uongozi wa Dayosisi unavyo treat walimu, na wanafunzi wasivyo na heshima kwa walimu wao baada ya kugundua kwamba hawathaminiwi, shule hii mwisho wake itakufa kabisa.

    ReplyDelete