Friday, April 20, 2012

HUU NDIO USAFIRI WETU NGARA

Kwa wale waliozoea usafiri wa mijini,hali inakuwa tofauti wanapokuja Ngara kqwani hali ya usafiri iko tofauti kabisa.

Gari ambayo kwa sehemu nyingine hupakia watu wasiozidi wanne,hapa kwetu inaweza kupakia watu zaidi ya 12,huku wengine wakikaa kwenye buti(sehemu ya kuwekea mizigo).

Nauli kutoka Ngara mpaka Kabanga ni shilingi elfu mbili kwa mtu mmoja,na kuna wakati wanapanda watu 15 kwenye hicho hicho kigari kidogo chenye uwezo wa kubeba abiria wanne.

Seat au kiti anachokalia dereva,hulazimika kukaa watu wawili kitu ambacho ni hatari sana kwani kinaweza kusababisha ajali.
hii ndiyo hali halisi

Kuna watu wamekuwa wakileta HIACE lakini muda c mrefu hukata tamaa kutokana na abiria kutaka kupanda gari ambalo halikai muda mrefu stand likisubiri abiria

BIASHARA YA MATUNDA ITAWANUFAISHA WENGI SANA NGARA

Kwa sasa wananchi wengi wa wilaya ya Ngara wamesitisha shughuli zao za kawaida na kuhamia katika biashara ya kusafirisha matunda kama vile maparachichi na ndizi za kisasa au ndizi kubwa.

Matunda hayo husafirishwa kwenda mikoa ya kanda ya kati (Dodoma na Singida)ambapo mfanyabiashara anaweza kupata faida ya zaidi ya shilingi elfu arobaini kwa gunia moja.

Gunia moja la maparachichi linaweza kupatikana katika vijiji vya wilayani Ngara kwa gharama isiyozidi  elfu kumi,ambapo bei ya kusafirisha gunia moaj kufika Dodoma ni shilingi elfu tano,na mzigo ukishafika Dodoma unauzwa kwa bei isiyopungua elfu hamsini kwa gunia moja,na mzigo ukifika Dodoma hauzungushwi,ndani ya masaa 12 mzigo unakuwa umekwisha tena kwa kugombaniwa.

je,ukipakia gunia ishirini unapata faida ya bei gan?

mzigo ukipakiwa kwenye lori kwa ajili ya kusafirishwa kuelekea Dodoma
Hali ya usafiri ndiyo rahisi sana kwani kuna maroli mengi yanatoka Burundi kwenda DAR,so hii ni biashara ambayo watu wengi wanaidharau lakini inalipa saaana.

Wednesday, April 18, 2012

JAMBAZI AUWAWA NA POLISI


Diwani wa kata ya Kabanga MH SAID SOUD
Jeshi la polisi wilayani Ngara limemuua mtu anayedhaniwa kuwa jambazi aliyekuwa na bomu la kutupwa kwa mkono

Diwani wa kata ya Kabanga Bw. Said Ramadhani Soud amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Nzaza baada ya kundi la majambazi  kutoka Burundi kuvamia katika kijiji cha Murukukumbo

Amesema jeshi la polisi kituo cha kabanga lilipata taarifa hizo ambapo waliwafuatilia na kumuua jambazi huyo baada ya tukio la kurushiana risasi na majambazi hao.

Amesema jambazi aliyeuwawa amefahamika kwa jina la Erick Ndabiholele mwenyeji wa wilaya ya Murama nchini Burundi

Amesema Polisi wamepata vitu vyenye thamani ya shilingi laki mbili ikiwa ni pamoja na simu tatu za mkononi zilizokuwa zimeibwa na watu hao

Kata ya Kabanga imekuwa ikikumbwa sana na vitendo vya ujambazi wa kutumia silaha siku za hivi karibuni,ambapo zaidi ya watu wawili wameuwawa na majambazi hao tangu mwanzoni mwa mwaka huu,na inasemekana majambazi hao wanatoka nchi jirani ya Burundi

Tuesday, April 17, 2012

AMBULANCE NGARA

Halmashauri ya wilaya ya Ngara imenunua piki piki za magurudumu matatu zitakazokuwa zikifanya huduma ya kuwasafirisha wanawake wajawazito kutoka vijijini kuwapeleka sehemu za barabarani ambapo watakuwa wakichukuliwa na magari kuelekea katika hospitali kubwa za wilaya kwa ajili ya kupatiwa huduma za kiafya.

Akiongea na NGARALIVE Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Ngara Dk.David Mapunda,amesema piki piki hizo tatu zitapangiwa vituo ambavyo zitakuwa zikikaa,japo kwa sasa vityuo hivyo bado havijabainishwa.

mojawapo ya piki piki hizo ikiwa imeegeshwa katika hospitali ya Nyamiaga ikisubiri kupangiwa kituo.Hii itafika kweli Ntobeye kupitia njia ya Murgwanza?
Dk.Mapunda ameongeza kuwa piki piki hizo ni kwa ajili ya wajawazito pekee tofauti na dharula nyingine zinazoweza kujitokeza

MVUA SIKU TATU MFULULIZO

Eneo kubwa la wilaya ya Ngara kwa siku tatu mfululizo limekuwa likitawaliwa na hali ya hewa ambayo sio nzuri sana.

Asubuhi ukiamka ukungu umetanda sehemu zote na manyunyu yasiyoonyesha dalili ya kukatika.

Hii imepelekea baadhi ya watu kusimamisha shughuli zao sanasana wale wa usafiri wa boda boda na sekido.

Hiyo ndo hali halisi inayoendelea hapa Ngara ambapo kwa muda wa siku tatu jua limekuwa adim sana.

BREAAKING NEEEWWZZZZ

ALEX GASHAZA ATANGAZA KUGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA NGARA.

Kada wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Ngara  Bw Alex Gashaza ametangaza rasmi kugombea uenyekiti wa wilaya wa chama hicho.

Bw.Gashaza ambaye amewahi kushiriki katika chaguzi kadhaa za ubunge wa jimbo la Ngara kupitia tiketi ya CCM mara mbili na mara moja kupitia tiketi ya NCCR Mageuzi,ameweka uamuzi huo hadharani katika kikao cha madiwani wa chama cha Mapinduzi kilichofanyika katika ofisi za CCM mjini Ngara.

Uchaguzi wa nafasi mbali mbali ndani ya CCM unafanyika mwaka huu ambapo kwa hivi sasa nafasi hiyo ya mwenyekiti inashikiliwa na Bi.Helena Adrian ambaye anamiliki shule ya RHEC iliyoko Rulenge

Monday, April 16, 2012

WANAFUNZI SITA TU DARASA ZIMA

jengo la utawala la shule ya sekondari MCHUNGAJI MWEMA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida shule ya Sekondari inayomilikiwa na kanisa la Anglikana dayosisi ya Kagera,MCHUNGAJI MWEMA,Imeonekana kupoteza kabisa mvuto kwa jamii baada ya shule hiyo kuwa na wanafunzi sita peke yao walioingia kidato cha kwanza mwaka huu shuleni hapo.

wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari MCHUNGAJI MWEMA wakiendelea na mjadala wa kimasomo darasani
Habari zilizoifikia NGARALIVE zinasema kuwa uhaba huo wa wanafunzi wanaojiunga na shule hiyo umepelekewa na matokeo mabovu ya kidato cha nne kwa mwaka jana hali ambayo imewakatisha tamaa wazazi.


Nao wanafunzi wa shule hiyo wamesema kuwa hali hiyo inachangiwa na kutokuwepo na maelewano mazuri kati ya waalimu wa shule hiyo na uongozi wa Dayosisi ya Kagera ambao ndio wamiliki wa shule hiyo.

LORI LAANGUKA,LAFUNGA BARABARA IENDAYO BURUNDI



Zaidi ya Malori 40 yaliyokuwa yakipeleka mizigo katika nchi za Burundi na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo,yamejikuta yakikwama kwa muda wa masaa zaidi ya 18 katika kijiji cha Murugarama baada ya Lori moja wapo kuanguka na kufunga barabara.

Lori hilo lenye namba za usajiri T 700 BFS lilianguka majira ya saa nane mchana siku ya jumapili April 15 katika kijiji cha Murugarama eneo la Njiapanda ya Rulenge,ambapo lilikuwa likipeleka mahindi nchini Burundi,na baada ya kuanguka lilifunga barabara hiyo hali iliyopelekea magari mengi hasa malori kukosa njia ya kupita kwa masaa kadhaa.

Watu walioshuhudia ajali hiyo wamesema kuwa chanzo chake ni mwendo wa kasi wa gari hilo,pamoja na mvua iliyokuwa ikinyesha kwa muda mrefu katika eneo hilo na kusababisha utelezi.

Hata hivyo watu waliokuwa katika gari hilo walisalimika ambao ni dereva na utingo.

Gari hilo awali likuwa likimilikiwa na Bw.Tenth Maruhe mkazi wa mjini Ngara kabla ya kuliuza kwa Mbarakk wa Biharamulo.

jitihadazikiendelea za kuliondoa barabarani
Baada ya madereva hao kuona hakuna jitihada zozote zinazofanywa na mamlaka husika kuondoa gari hilo barabarani,walishirikiana wao wenyewe na kulitoa ambapo shughuli za usafirishaji katika barabara hiyo zimelejea katika hali ya kawaida.
hivi ndivyo lilivyokaa baada ya kuanguka

wananchi wakishirikiana kuinua tela la lori hilo
Ajali hiyo ni ya pili kutokea katika eneo hilo kwa kipindi cha miezi miwili,ambapo mwezi wa pili watu wawili walipoteza maisha baada ya kugongwa na roli katika eneo hilo hilo.