Tuesday, June 12, 2012

TUNABADILI JINA

Nawashukuru wadau wote wa NGARALIVE kwa kuendelea kuwa karibu na BLOG yenu ili kupata taarifa mbali mbali zinazojili wilayani kwetu.Hata hivyo nasikitika kuwataarifu kuwa kwa sasa nabadili jina na maudhui ya BLOG hii.Nimelazimika kufanya hivyo kutokana na kuhamisha makazi yangu.Awali nilikuwa wilayani Ngara lakini kwa sasa nahamia Mkoani MWANZA kikazi,hivyo haitakuwa rahisi mimi kupatra kile kinachojiri NGARA kwa wakati husika.
Kwa hali hiyo nitakuwa naweka taarifa za kitaifa,japo na zile za NGARA zitakuwa zinapewa kipaumbele,kwa hiyo tegemeeni kuona mabadiliko ya taarifa kutoka NGARALIVE inayobadilika kuwa DOXLIN JASSON.BLOGSPOT.COM
ASANTENI...........

Wednesday, May 16, 2012

CAPTAIN BRIAN BGOYA AFARIKI DUNIA

Captain Brian Niyimpa Bgoya(pichani) amefariki dunia katika hospitali ya HINDU MANDAL jijini Dar es Salaam tarehe 13 MAY mwaka huu.

Mazishi yatafanyika siku ya Jumamosi MAY 15 nyumbani kwao Mubinyange Ngara ambapo mwili wa marehemu unatarajiwa kufikishwa Ngara siku ya Ijumaa.

NGARA LIVE INATOE POLE KWA WOTE WALIOFIKWA NA MSIBA HUO

Wednesday, May 9, 2012

WILAYA YA NGARA YAPATA MKUU WA WILAYA MPYA

Wilaya ya Ngara imepangiwa Mkuu wa Wilaya mpya,atakayechukua nafasi ya Kanali Mstaafu Salum Nyakonji.
Kwa mujibu wa uteuzi mpya wa Wakuu wa Wilaya,nafasi hiyo hapa wilayani Ngara itachukuliwa na COSTANTINE J.KANYASU.
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara Kanali Mstaafu Salum Nyakonji,kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe
Hata hivyo taarifa hiyo ya awali haikueleza kama kuna kituo kingine alichopangiwa KANALI NYAKONJI.

Wafuatao ndio Wakuu wapya wa wilaya na vituo vyao vya kazi
1. Novatus Makunga Hai
2. Mboni M. Mgaza Mkinga
3. Hanifa M. Selungu Sikonge
4. Christine S. Mndeme Hanang
5. Shaibu I. Ndemanga Mwanga
6. Chrispin T. Meela Rungwe
7. Dr. Nasoro Ali Hamidi Lindi
8. Farida S. Mgomi Masasi
9. Jeremba D. Munasa Arumeru
10. Majid Hemed Mwanga Lushoto
11 Mrisho Gambo Korogwe
12. Elias C. J. Tarimo Kilosa
13. Alfred E. Msovella Kiteto
14. Dkt. Leticia M. Warioba Iringa
15. Dkt. Michael Yunia Kadeghe Mbozi
16. Mrs. Karen Yunus Sengerema
17. Hassan E. Masala Kilombero
18. Bituni A. Msangi Nzega
19. Ephraem Mfingi Mmbaga Liwale
20. Antony J. Mtaka Mvomero
21. Herman Clement Kapufi Same
22. Magareth Esther Malenga Kyela
23. Chande Bakari Nalicho Tunduru
24. Fatuma H. Toufiq Manyoni
25. Seleman Liwowa Kilindi
26. Josephine R. Matiro Makete
27. Gerald J. Guninita Kilolo
28. Senyi S. Ngaga Mbinga
29. Mary Tesha Ukerewe
30. Rodrick Mpogolo Chato
31. Christopher Magala Newala
32. Paza T. Mwamlima Mpanda
33. Richard Mbeho Biharamulo
34. Jacqueline Liana Magu
35. Joshua Mirumbe Bunda
36. Constantine J. Kanyasu Ngara
37. Yahya E. Nawanda Iramba
38. Ulega H. Abadallah Kilwa
39. Paul Mzindakaya Busega (mpya)
40. Festo Kiswaga Nanyumbu
41. Wilman Kapenjama Ndile Mtwara
42. Joseph Joseph Mkirikiti Songea
43. Ponsiano Nyami Tandahimba
44. Elibariki Immanuel Kingu Kisarawe
45. Suleiman O. Kumchaya Tabora
46. Dkt. Charles O. F. Mlingwa Siha
47. Manju Msambya Ikungi (mpya)
48. Omar S. Kwaangw’ Kondoa
49. Venance M. Mwamoto Kibondo
50. Benson Mpesya Kahama
51. Daudi Felix Ntibenda Karatu
52. Ramadhani A. Maneno Kigoma
53. Sauda S. Mtondoo Rufiji
54. Gulamhusein Kifu Mbarali
55. Esterina Kilasi Wanging’ombe (mpya)
56. Subira Mgalu Muheza
57. Martha Umbula Kongwa
58. Rosemary Kirigini Meatu
59. Agness Hokororo Ruangwa
60. Regina Chonjo Nachingwea
61. Ahmed R. Kipozi Bagamoyo
62. Wilson Elisha Nkhambaku Kishapu
63. Amani K. Mwenegoha Bukombe
64. Hafsa M. Mtasiwa Pangani
65. Rosemary Staki Senyamule Ileje
66. Selemani Mzee Selemani Kwimba
67. Lt. Col. Ngemela E. Lubinga Mlele (mpya)
68. Iddi Kimanta Nkasi
69. Muhingo Rweyemamu Handeni
70. Lucy Mayenga Uyui

Tuesday, May 8, 2012

AJALI YAUA WAWILI K 9


Mteremko wa K 9 umezidi kuwa tishio hasa kwa madereva wa maroli baada ya hivi karibuni lori moja kufail break kisha kuacha njia na kuua watu wawili papo hapo.

Dereva wa Lori hilo lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Burundi,ni mmoja kati ya waliopoteza maisha.
Mwingine ni mwendesha piki piki ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kasharazi,yeye alikuwa barabarani ambapo gari hilo lilimpitia katika harakati za kuacha njia.

hiyo ni sehemu ya CABIN ya lori hilo
kwa mbali hiyo inayoonekana ndiyo piki piki iliyogongwa ikiwa chini ya gari hilo
hivyo ndivy lilivyokuwa
hilo ndilo container la gari hilo,lenyewe lilichomoka na kuporomoka zaidi ya mita mia moja hamsini,na ndani ya container hilo kulikuwa na gari jipya aina ya FUSO
Utingo wa Lori hilo alishuka kuweka kigingi baada ya kuona kuwa limefail break,hivyo yeye hakuweza kupata jeraha lolote.

Tuesday, May 1, 2012

HIKI NDICHO SHULE ZETU ZA NGARA ZILICHOKIVUNA KATIKA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2012


S0611 KABANGA SECONDARY SCHOOL

DIV-I = 1 DIV-II = 9 DIV-III = 36 DIV-IV = 10 FLD = 1 

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

S0397 RULENGE SECONDARY SCHOOL

DIV-I = 1 DIV-II = 4 DIV-III = 19 DIV-IV = 10 FLD = 1 

 ++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

S4419 LUKOLE SECONDARY SCHOOL

DIV-I = 1 DIV-II = 25 DIV-III = 59 DIV-IV = 4 FLD = 0 

+++++++++++++++++++++++++++++++++

 

Friday, April 20, 2012

HUU NDIO USAFIRI WETU NGARA

Kwa wale waliozoea usafiri wa mijini,hali inakuwa tofauti wanapokuja Ngara kqwani hali ya usafiri iko tofauti kabisa.

Gari ambayo kwa sehemu nyingine hupakia watu wasiozidi wanne,hapa kwetu inaweza kupakia watu zaidi ya 12,huku wengine wakikaa kwenye buti(sehemu ya kuwekea mizigo).

Nauli kutoka Ngara mpaka Kabanga ni shilingi elfu mbili kwa mtu mmoja,na kuna wakati wanapanda watu 15 kwenye hicho hicho kigari kidogo chenye uwezo wa kubeba abiria wanne.

Seat au kiti anachokalia dereva,hulazimika kukaa watu wawili kitu ambacho ni hatari sana kwani kinaweza kusababisha ajali.
hii ndiyo hali halisi

Kuna watu wamekuwa wakileta HIACE lakini muda c mrefu hukata tamaa kutokana na abiria kutaka kupanda gari ambalo halikai muda mrefu stand likisubiri abiria

BIASHARA YA MATUNDA ITAWANUFAISHA WENGI SANA NGARA

Kwa sasa wananchi wengi wa wilaya ya Ngara wamesitisha shughuli zao za kawaida na kuhamia katika biashara ya kusafirisha matunda kama vile maparachichi na ndizi za kisasa au ndizi kubwa.

Matunda hayo husafirishwa kwenda mikoa ya kanda ya kati (Dodoma na Singida)ambapo mfanyabiashara anaweza kupata faida ya zaidi ya shilingi elfu arobaini kwa gunia moja.

Gunia moja la maparachichi linaweza kupatikana katika vijiji vya wilayani Ngara kwa gharama isiyozidi  elfu kumi,ambapo bei ya kusafirisha gunia moaj kufika Dodoma ni shilingi elfu tano,na mzigo ukishafika Dodoma unauzwa kwa bei isiyopungua elfu hamsini kwa gunia moja,na mzigo ukifika Dodoma hauzungushwi,ndani ya masaa 12 mzigo unakuwa umekwisha tena kwa kugombaniwa.

je,ukipakia gunia ishirini unapata faida ya bei gan?

mzigo ukipakiwa kwenye lori kwa ajili ya kusafirishwa kuelekea Dodoma
Hali ya usafiri ndiyo rahisi sana kwani kuna maroli mengi yanatoka Burundi kwenda DAR,so hii ni biashara ambayo watu wengi wanaidharau lakini inalipa saaana.